Wajumbe wa Bodi ya Jumuiya ya Watoa Huduma katika Sekta ya Mafuta na Gesi Tanzania (#ATOGS) ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi Hon. Abdulsamad Abdulrahim, Wakurugenzi wa Bodi, Wajumbe wa Kamati pamoja na Sekretariat walifanya mazungumzo na Uongozi wa Wizara ya Nishati (#MoE) ukiongozwa na Kaimu Katibu Mkuu Mhe. Adam Zuberi pamoja na Maafisa wa Wizara.

Pamoja na mambo mengine, lengo kuu la mkutano huo lilikuwa ni kuitambulisha rasmi Bodi na Menejimenti ya #ATOGS kwa Uongozi wa Wizara ya Nishati uliopo.

Katika Kikao hicho #ATOGS pamoja na Wizara ya Nishati walijadili mambo mbalimbali ikiwemo:-

1. Maboresho ya sheria mbalimbali zinazotekelezeka katika Sekta ya Mafuta na Gesi nchini,

2. Kuwepo kwa Sera nzuri na rafiki ili Kuwavutia Wawekezaji (Investors) nchini,

3. Malengo ya #ATOGS na Utawala Bora (Good Governance) katika Sekta ya Mafuta na Gesi Tanzania,

4. Ushirikishwaji wa Wazawa (#LocalContent) katika miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ili kuhakikisha Wazawa Wanapewa vipaumbele katika fursa zilizopo kwenye miradi ili kuendelea kukuza uchumi wa nchi na kuboresha maisha ya kila Mtanzania,

5. Kuendelea kukuza na kuboresha mahusiano mazuri kati ya Sekta binafsi na Serikali nchini.

Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya #ATOGS, Mhe. Abdulsamad Abdulrahim alimuhakikishia Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhe. Adam Zuberi kuwa #ATOGS ipo tayari kushirikiana na Wizara ya Nishati ili kuhakikisha Watanzania wananufaika na fursa zilizopo katika miradi yote ya Kimkakati na Uwekezaji inayotekelezwa na Serikali.

Pia, Mhe. Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhe. Adam Zuberi, alifurahishwa na ujio wa Bodi ya #ATOGS Wizarani, vile vile aliwahakikishia Wajumbe wa Bodi kwamba Serikali ipo tayari kushirikiana na Sekta binafsi nchini ili kusukuma gurudu la maendeleo yetu kwa pamoja.

Sekretariat,

Jumuiya ya Watoa Huduma katika Sekta ya Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS),
Simu: +255 746 376 306 / +255 769 626 044
Barua Pepe: [email protected]